Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji Jacob Mwambengele mapema Septemba 23, 2025 ametembelea Halmashauri ya Wilaya ya Iringa katika kijiji cha Mtera kata ya Migoli na kupokelewa na msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo la Kalenga na Ismani Bi. Caroline Utieno
Lengo la ziara ni kukagua na kuona hatua iliyofikiwa katika maandalizi ya Uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025 ambapo ameweza kupokea taarifa ya kazi zinazoendelea sanjari na maandalizi ya vifaa.
Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kupitia majimbo yake mawili, Kalenga na Ismani ina jumla ya kata 28, vijiji 134, vitongoji 745 na vituo vinavyotarajiwa kutumika kupigia kura ni 645 ambako kwenye maeneo yote hayo kazi na maandalizi mengine yanaendelea ikiwemo mikutano mbalimbali ya kampeni
Uchaguzi Mkuu wa Rais, wambunge na madiwani unatarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025 ambapo kauli mbiu inayotumika ni "kura yako haki yako, jitokeze kupiga kura"
#kurayakohakiyakojitokezekupigakura
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa