Mkurugenzi wa Elimu Idara ya Elimu Sekondari -OR TAMISEMI Mwl. Khadija Mcheka Leo ,Mei 31, 2024 Ameongea na walimu wa halmashauri ya wilaya ya Iringa akiwaomba walimu kuwa na mbinu wakati wa ufundishaji Kwani kupitia hivo itasaidia kuongeza ufaulu huku akiwasihi kutumia mbinu ya uwezo, utayari na kujua umri wa mtoto kuweza kujua njia ipi ya kufundisha.
Pia Mwl. Mcheka Amewasihi Maafisa Elimu na walimu kuwa na lugha nzuri kwani kupitia lugha nzuri husaidia kuwa karibu na watoto na kuweza kujua watoto Wana changamoto moto ipi huku akiwataka kuanza kufundisha vizuri Toka madarasa ya kwanza na kidato Cha kwanza kama kuwa na mafunzo ya lugha ya kingereza wiki 3 za mwazoni kwani msingi mzuri ukiwekwa kwenye madarasa ya Awali Ina saidia kupandisha Ufaulu.
Vile vile Mwl. Mcheka Amesema kuwa wanatambua changamoto za walimu ndo maana Mhe. Rais wa Jamuhri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Suluh Hassan Alikaa kikao na kutoa namba ya simu Kwa Ajili ya Kusikiliza Kero za Walimu kama vile Mundo wa walimu, hela za uhamisho na kupandishwa madaraja na lugha sisizo faa kwa walimu huku akielekeza Wizara ya Tamisemi kutolea majibu ya Changamoto Hizo.
Pamoja na hayo Mwl. Mcheka Amewahidi walimu wote kufikia Julai wenye Stahiki ya kupanda madaraja watakuwa tayari, huku akitolea ufanuzi kuhusu hela za uhamisho kuwa Halmashauri wameanza kulipa pamoja na hela za likizo.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa