Mwongozo wa Chakula na Ulaji Watolewa Tanzania Bara
Mwongozo huo umeweza kutolewa katika Kikao cha Kamati ya Lishe Robo ya Pili Oktoba – Desemba kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024, katika Ukumbi wa Halmashauri uliopo Ihemi Februari 16, 2024.
Kamati hiyo imeweza kupokea Muongozo wa Chakula na Ulaji Tanzania Bara, ambao umetolewa mwaka 2023 na ushauri wa Kitaalamu.
Akiwasilisha taarifa hiyo na Muongozo Afisa Lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Bi. Tiliza Mbulla amesema, “lengo la muongozo huu ni kuboresha hali ya lisha na afya za watu wa rika na makundi yote katika jamii ya Watanzania. Pia Dahamira hii inadhihirishwa katika Sera, mikakati, mipango ya maendeleo na afua mbalimbali zinazokusudia kupunguza aina zote za utapiamlo”.
Bi. Tiliza ameendelea kusema, “kuna miongozo mbalimbali imetolewa ili kuleta ufanisi kama, kula vyakula mchanganyiko kutoka makundi sita ya chakula kila siku, kujitahidi kufikia lishe inayopendekezwa kwa akina mama wajawazito na wanaonyonyesha, watoto wachanga wadogo ili kuhakikisha afya bora ya mama na mtoto, kupunguza ulaji wa vyakula vilivyokaangwa na mafuta mengi, kuhakikisha usafi wa mazingira wa mahali unapoishi na usalama wa chakula, kuwa na mtindo bora wa maisha ili kupata afya bora na uzito unaoshauriwa, kuepuka tabia hatarishi kama vile uvutaji wa sigara na unywaji wa pombe”.
Kamati pia imeweza kupokea taarifa za utekelezaji kwa kipindi cha Oktoba – Desemba kutoka Idara mbalimbali zilizopo kwenye mpango wa Afua za Lishe ambazo ni Idara ya Afya, Idara ya Elimu ya Awali na Msingi, Idara ya Elimu Sekondari, Idara ya Kilimo na Idara ya Maendelo ya Jamii.
Idara hizo zimeweza kubainisha changamoto mbalimbali kama, kuendelea kuwepo kwa matatizo ya lishe kama uzito pungufu, ukondefu na upungufu wa damu kwa wajawazito, baadhi ya shule hazikupanga bajeti ya kuanzisha mashamba ya kilimo cha mazao lishe na miti ya matunda, ushiriki mdogo wa wakulima katika mafunzo kutokana na shughuli za msimu wa kilimo, uelewa mdogo wa uhifadhi wa chumvi yenye madini joto, baadhi ya wazazi/walezi kutowajibika ipasanvyo kuwaandlia watoto chakula kwa wakati kwa kuendekeza ulevi, baadhi ya Kaya kushindwa kumudu milo mitatu kwa siku, muitikio wa wanaume katika masuala ya lishe hasa kwenda kliniki na kushiriki siku za lishe za vijiji.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa