Shirika la Nyumba la Taifa(NHC) latoa madawati 34 katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ambayo yamekabidhiwa Shule ya Sekondari Kidamali iliyopo kata ya Nzihi. Zoezi la makabidhiano haya limeongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Mhe. Steven Mhapa Agosti 15, 2024.
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya viti na meza katika shule ya Sekondari Kidamali Mh. Mhapa amesema, “Tumepokea kwa moyo wa dhati na shukrani kubwa sana msaada huu ambao ni kwa ajili ya watoto wetu hawa hongereni sana”
Aidha ameongeza kuwa maendeleo mara zote huletwa kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali kwani sio Serikali tu ndio inayoweza kufanya kila kitu hivyo kama kuna watu wanajitokeza kuunga mkono na kufanya vitu lazima watambuliwe kwa jitihada zao hizo.
Kwa upande mwingine Mhe. Mhapa ametoa rai kwa wanafunzi, na walimu kuhakikisha kuwa madawati hayo (viti na meza) yanatunzwa ipasavyo.
Naye Mkurugenzi wa NHC (Kitengo cha Ubunifu na utaalamu katika majengo) Mhandisi Emmanuiel Moshi Amesema kazi kubwa ya Shirika la Nyumba la Taifa ni kuigusa jamii kwa kuipatia makazi ya aina mbalimbali ambapo mbali na hapo ni kuigusa jamii kwa namna nyingine kwa kutumia kile kinachopatikana kutokana na kazi ya msingi kama ambavyo imefanyika hapa ya kutoa msaada wa samani hizi (viti na meza).
Kwa upande wake Afisa Elimu Sekondari Bi. Alice Nkwera amewapongeza na kuwashukuru wadau wa maendeleo (NHC) kwa moyo wao wa kuchangia uborehaji wa miundombinu ya elimu kama ambavyo wametoa madawati 34 kwa Shule ya Sekondari Kidamali na kuishukuru pia Serikali inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Mgao mkubwa wa madarasa ambapo shule ya sekondari kidamali imeweza kupata vyumba 3 vya madarasa yenye thamani ya Shilingi Milioni 75.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa