OFISI ZA IRINGA DC KUHAMIA IHEMI MWISHONI MWA MWEZI JULAI 2023
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Wakili Bashir Muhoja tarehe 14.07.2023 amefanya kikao na watumishi wote wa makao makuu ya Halmashauri ikiwa ni maandalizi ya kuhamia katika ofisi mpya zilizopo katika kijiji cha Ihemi.
Akizungumza wakati wa kikao, Wakili Muhoja amesema kuwa Mkuu wa Mkoa alitoa agizo la kuhamia kwenye Jengo la Halmashauri la Ihemi ifikapo tarehe 30 Julai, 2023 hivyo agizo hilo lazima litekelezwe na sasa ni rasmi kuwa kuanzia tarehe 31 July, 2023 huduma zote za kiofisi zitaanza kutolewa kwenye Ofisi Mpya zilizopo kwenye Jego la Halmashauri lililopo Ihemi.
Amesema pamoja na changamoto zilizopo kule ikiwa ni pamoja na changamoto ya makazi kwa watumishi lakini Serikali imewekeza fedha nyingi kwenye ule ujenzi na kwa asilimia kubwa kazi imekamilika hivyo watumishi wajiandae kwenda.
Sambamba na agizo hilo la kuhamia Ihemi vilevile Serikali itazingatia maslahi ya watumishi wote watakaohamia kama ambavyo yapo kwa muujibu wa sheria na kwamba taratibu za kiutumishi zifuatwe ili kila mmoja apate haki yake.
Kwa upande wao baadhi ya watumishi walitaka kujua kuhusu utatuzi wa changamoto zinazoweza kujitokeza kule ikiwa ni pamoja na upungufu wa vyumba vya ofisi, upungufu wa makazi kwa watumishi, na suala la maji, mambo ambayo pia yameweza kutolewa ufafanuzi.
Wakili Muhoja amewatoa hofu watumishi kwa kueleza kuwa changamoto zote zimechukuliwa kwa uangalifu mkubwa ikiwemo suala la maji na upungufu wa vyumba vya ofisi, aidha kwa upande wa makazi kwa watumishi ameshauri watumishi wapangishe nyumba /vyumba kwenye maeneo ya jirani mfano Ifunda na Tanangozi wakati jitihada mbalimbali zikifanyika ili kupata makazi kwa watumishi.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa