RC Dendego Ahimiza Uharakishwaji wa Ujenzi wa Miradi ya BOOST
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mheshimiwa Halima Dendego amefanya ziara katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ya kukagua miradi mbalimbali Juni 14, 2023 kwa lengo la kujionea maendeleo ya miradi hiyo.
Mheshimiwa Dendego aliendelea na ziara katika Kata ya Ifunda Kijiji cha Ifunda, na kukagua mradi wa ujenzi wa shule mpya ya Msingi ya Kibaoni ambapo ipo katika hatua ya msingi. Mradi huo unatekelezwa na Program ya BOOST, na inakadadiriwa kutumia kiasi cha Shilingi Milioni 300 hadi kukamilika kwake.
Mheshimiwa Dendego ametoa maagizo katika mradi huo na kusema kuwa, “mradi umechelewa kuanza na kufanya siku zilizopangwa kukamilika kwa mradi ziwe chache. Hivyo kuanzia sasa nataka watendaji wote wawe eneo la ujenzi usiku na mchana ili mradi ukamilike kwa wakati kama ilivyopangwa”.
Kadhalika Mheshimiwa Dendego ametembelea mradi wa bwawa la Samaki lililopo katika Kijiji cha Makota Kata ya Masaka na kuweza kupanda vifaranga vya Samaki 9000 katika bwawa hilo, akiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Komredi Daudi Yassin Mlowe ikiwa ni agizo la Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Taifa Mheshimiwa Daniel Chongolo, la kuongeza idadi ya vifaranga vya Samaki kwenye bwawa hilo, alipotembelea mwishoni mwa mwezi Mei 2023 na akapanda vifaranga vya Samaki 3000 na kufanya jumla ya vifaranga vilivyopandwa kuwa 12,000.
Aidha Mheshimiwa Dendego amekagua mradi wa utengenezaji wa barabara na kivuko kinachounganisha Kijiji cha Ifunda na Ulole, ambapo mradi huo unatekelezwa na Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini – TASAF kupitia walengwa wanaonufaika na mpango huo. Barabara hiyo yenye urefu wa Mita 200 na kivuko itapunguza kero kwa watumiaji wa Kijiji cha Ifunda na Ulole.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri Mheshimiwa Stephen Mhapa, amemuhakikishia Mheshimiwa Dendego kuwa, atasimamia na kufuatilia kila hatua katika utekelezaji wa miradi hiyo, ili iweze kukamilika kwa wakati.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa