RC Dendego Azitaka Halmashauri za Mkoa wa Iringa kutumia Takwimu za Sensa katika Mipango ya Maendeleo
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Halima Dendego amezitaka Halmashauri za Mkoa wa Iringa kutumia takwimu za sensa za mwaka 2022 katika mipango ya bajeti za Halmashauru na kuapanga mipango ya maendeleo kwa wananchi.
Matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwka 2022 ni kwa ajili ya mipango jumuishi na maendeleo endelevu ya Taifa letu ambayo yataongeza uwazi katika kupanga rasilimali zilizopo kulingana na uwiano wa idadi ya watu katika ngazi mbalimbali.
Amesema.Ameyasema hayo alipokuwa akufungua kikao cha kamati ya ushauri ya Mkoa kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023, kilichofanyika leo Januari 11, 2022 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa (Siasa ni Kilimo).
Mhe. Dendego amesema Mkoa wa Iringa ni miongoni mwa Mikoa inayoongoza kwenye uchangiaji wa pato la Taifa ikiwa ni ya pili baada ya Mkoa wa Dar es salaam lakini amesema ili kuendana na hilo inabidi maisha ya watu pia yaendane na pato la Mkoa.
Kwa mujibu wa Takwimu za Maendeleo za Ofisi ya Taifa ya Tamwimu (NBS) zilizotolewa mwaka 2021, pato la mwananchi kwa mwaka limefikia shilingi 4,028,000 kutoka 3,527,493.00.
"Haya ni mafanikio makubwa ya kujivunia, nawapongeza wananchi wa Mkoa wa Iringa kwa kuendelea kuzalisha na kukuza uchumi katika sekta za uzalishaji ni matarajio yangu makubwa kuwa kwa mwaka 2022/2023 kutakua na ongezeko kubwa la uzalishaji katika sekta mbalimbali za kiuchumi".
Aidha amesema Mkoa wa Iringa umeendelea kufanya vizuri kwenye huduma za jamii zikiwemo Elimu, Afya, Maji, Nishati ya Umeme, Miundombinu.
"Serikali imeendelea kuleta fedha nyingi na kwa wakati ili kuhakikisha kuwa shughuli zote zq kupeleka huduma kwa wananchi wake zinaendelea kwa kasi kubwa na kwa wakati".
Katika Kikao hicho pia amewaagiza viongozi wa ngazi zote kuendelea kuwaelimisha wananchi kuhusu changamoto ya mvua chache na kuwahamasisha kutumia vyema mvua zinazoendelea kunyesha kwa kupanda mazao ya muda mfupi.
Aidha amewaagiza viongozi wa kila Halmashauri kuendelea kuhamasisha shughuli za upandaji miti ikiwa ni kutekeleza agizo kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais la kupanda miti 1,500,000. Kila mwaka lakini pia kuzingatia upandaji miti rafiki wa maji kwenye maeneo ya vyanzo vya maji.
Pia Mkuu wa Mkoa amewapongeza Wadau na Wataalamu wa lishe kwa jitihada kubwa walizozifanya na wanaziendelea kuzifanya na kupelekea Mkoa kuibuka kidedea katika utekelezaji wa mkataba wa lishe.
“Katika utekelezaji wa mkataba wa lishe, Mkoa umefanikiwa kuibuka mshindi wa tatu (3) kitaifa na kupata tuzo, hii ni hatua nzuri na kubwa lakini bado tunapaswa kushirikiana na kuongeza juhudi ili kutokomeza kabisa udumavu na utapiamlo ndani ya mkoa wetu”.
Mkoa pia umejiwekea mikakati ya kukuza ajira kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu hivyo mikakati ni pamoja na kuwatambua walengwa walipo na mahitaji yao.
Pia kutenga asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauru kutoa mikopo kwa makundi hayo, kuweka mazingira wezeshi ya biashara na kilimo cha pamoja kwa vijana, kuibua fursa mbalimbali za uwezeshaji makundi hayo kupitia mabaraza yetu ya biashara ya Mkoa na Wilaya, TCCIA na Halmashauti, kuwajengea uwezo makundi hayo na kuwaunganisha na mifuko mingine ya fursa. Amesema Dendego.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa