Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba ametoa pongezi kwa kazi inayoendelea ya ujenzi wa mfereji wa umwagiliaji ya Ipwasi – Ndorobo katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Mhe. Serukamba ametoa pongezi hizo alipotembelea na kukagua kazi ya ujenzi wa mfereji huo sanjari na kuongea na mafundi mapema April 23, 2024.
Skimu ya Ipwasi – Ndorobo inajengwa kwa gharama ya Shilingi Milioni 62 zilizotolewa kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa mfereji huo. Huu ni mradi ambao unanufaisha wakulima zaidi ya 200 ambao wanalima mazao mbalimbali ikiwemo mpunga, mahindi na mazao ya mbogamboga.
Aidha, Mhe. Serukamba ametembelea na kukagua kazi kwenye miradi ya ujenzi wa uzio katika shule ya msingi Kipera, shule ambayo inahudumia watoto wenye mahitaji maalumu, ujenzi wa matundu 21 ya vyoo katika shule ya Sekondari Idodi, ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa katika Shule ya Msingi Idodi, ujenzi wa kituo cha Afya Mlenge, na kuongea na wananchi wa Ilolompya.
Katika ziara hii Mkuu wa Mkoa Mhe. Peter Serukamba amesisitiza ukamilishwaji wa miradi kwa wakati na Mhandisi wa Wilaya kusimamia na kuhakikisha kuwa idadi ya mafundi inaongezeka ili waweze kukamilisha kazi ya ujenzi kwa wakati.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa