RC IRINGA APONGEZA UTEKELEZAJI WA MIRADI IRINGA DC
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Halima Dendego amefanya ziara ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa Miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa tarehe 25.10.2023 na kutoa pongezi kwa usimamizi mzuri wa miradi hiyo.
Miradi iliyotembelewa na kukaguliwa ni
Mkuu wa Mkoa amemshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna fedha za miradi zinavyomiminika na kutoa wito kwa wananchi kumuunga mkono.
Akizungumza wakati wa kukagua ujenzi wa shule ya sekondari ya kata ya Ulanda(Weru) Mhe. Dendego amesema, “Kwa fedha zote hizi zinazomiminika kwenye miradi, tumpe zawadi Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan kwa Kumuunga mkono”.
Pia Mhe Dendego ametoa pongezi kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Wakili Bashir Muhoja kwa utendaji na usimamizi makini wa miradi sanjari na makundi mengine yaliyochangia kufanikisha kazi.
Kwa upande wa uwezeshwaji kiuchumi kwa akinamama na vijana, Mhe. Dendego ametoa agizo kuwa 60% ya mikopo yote ielekezwe vijijini na asilimia 40% itabaki kwenye miji midogo na miji mikubwa na kwamba vijijini wanahitaji tu elimu na uwezeshwaji ili mambo yao yaende.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Wakili Bashir Muhoja amesema shule ya sekondari ya kata ya Ulanda(Weru) tayari imeshapata usajili na mipango iliyopo ni kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza na cha pili ili kuwapunguzia wanafunzi adha ya kutembea umbali mrefu hadi Kalenga.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa