Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Halima Dendego amezindua rasmi kampeni ya kupinga udumavu na kumtua mama kuni kichwani wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika kimkoa katika viwanja vya Samora Manispaa ya Iringa Machi 8, 2024.
“Mkoa wetu tuna changamoto kubwa ya udumavu, kwa mujibu wa takwimu na tafiti zilizofanywa udumavu Iringa ni 56.6%. Ni Mkoa wa kwanza unaozalisha watoto wenye udumavu chini ya miaka mitano, leo tunaenda kukata utepe tunasema Iringa bila udumavu inawezekana” amesema Mhe. Dendego.
Aidha Mhe. Dendego amesema kuwa kinara namba moja wa kampeni hii ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amechukua hatua kwa kuwasainisha mikataba wakuu wa Mikoa, kisha wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na viongozi wa kata na vijiji, hivyo jambo hili ni la kuzingatiwa sana (very serious) na ni jukumu la kila mmoja.
Sanjari na hayo, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa maagizo ya kumtua mama kuni kichwani hivyo kama utekelezaji Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Halima Dendego amezindua kampeni hiyo na kuitaka jamii kuachana na matumizi ya kuni na mkaa badala yake jamii itumie nishati mbadala ambayo ni nishati safi yaani umeme, sola, gesi na mkaa mweupe wa viwandani.
Mhe. Dendego pia amewaasa wanawake kuungana na akina baba kusimamia maendeleo kwa kushiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu 2024.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa