Saida Mgeni Afunga Mafunzo ya Utaji Mikopo Yafungwa
Mafunzo ya utoaji mikopo ya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu (10%), yalianza Oktoba 01 ambayo yametolewa kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii yamehitimishwa Oktoba 05, 2024. Wakati yamehitimishwa Watendaji wa Kata na Maafisa Tarafa walikuwepo ili kupewa majukumu nini wanatakiwa kufanya na kuzingatia wakati wa utoaji mikopo hiyo.
Akizungumza katika mafunzo hayo Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa Bi. Saida Mgeni amesema,” nawasihi mkasimamie vizuri kazi hii ya utoaji mikopo kwa wananchi, ili tusimuangushe Mheshimiwa Rais ambaye ametoa fedha hizo. Pia endeleeni kufuatilia marejesho ya mikopo ya nyuma ambayo hadi sasa bado haijarejeshwa. Kwa kushirikiana ninyi Maafisa Tarafa, Watendaji wa Kata na Maafisa Maendeleo ya Jamii tutafanya vizuri kwani ninyi ndiyo mnawajua vizuri wananchi walio katika maeneo yenu”
Naye Afisa Mwandamizi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Nchini Ndugu Ditram Muhoma amewaambia Maafisa hao kuwa, kama zilivyo kwenye kazi nyingine za Kitaifa na hii ya utoaji wa mikopo ni ya Kitaifa pia, hivyo zingatieni uadilifu kwa kila kikundi kinachokopa.
Ndugu Muhoma ameendelea kusema kuwa, “ukikamatwa unahujumu mikopo kwa kupitisha vikundi visivyo na sifa basi utakuwa umeingia katika sifa ya kuhujumu uchumi”.
Ameowaomba kuzingatia thamani ya fedha zinazotolewa na Mheshimiwa Rais pia ni vizuri kutolea taarifa kwa kila kikundi kinachokopa.
Kwa upande wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Kiasi cha Shilingi Milioni 762 zimetengwa kwa ajili ya kutolewa kwa vikundi hivyo kwa njia ya mkopo.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa