Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Kheri James ameongoza viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa na viongozi wengine wa Chama cha Mapinduzi kutoa mkono wa pole kwa wahanga wa mvua iliyoambatana na upepo mkali katika kata ya Itunundu na Mlenge tarafa ya Pawaga – Iringa Machi 25, 2025.
Mhe. James amekabidhi vyakula, magodoro, mablanketi na vifaa vya ujenzi kwa waathirika kwa upepo ambao nyumba zao ziliharibiwa na kupelekea kukosa makazi na mahitaji mengine ya kibinadamu.
Akizungumza wakati wa ugawaji wa vifaa hivyo Mhe. James ametoa pole kwa wakazi wa Pawaga kufuatia kadhia waliyoipata na kutoa pongezi kwa Serikali, viongozi na wananchi wengine sanjari na ofisi ya Mbunge Mhe. William Lukuvi waliochukua hatua za haraka kutoa msaada uliohitajika.
Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Dkt. Samweli Marwa akitoa taarifa ya maafa hayo amesema kuwa jumla ya kaya 241 ambazo zilikuwa na watu1436 zimeathirika ndani ya vijiji saba vya kata ya Itunundu na Mlenge. Pia ameongeza kuwa Jumla ya vifo 3 vimetokea pamoja na majeruhi 7 ambao waliweza kuhudumiwa haraka na kurejea kwenye maeneo yao.
Kwa upande wao wananchi pamoja na viongozi mbalimbali wa Pawaga wametoa shukrani kwa Serikali inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa hatua za haraka kutoa msaada kwa waathirika wa tukio hilo na kupokea vema msaada huo.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa