Timu ya Mbugani Yaibuka Kidedea MBOMIPA CUP 2022
Timu ya mpira wa miguu kutoka kijiji cha Mbugani Kata ya Mboliboli wameibuka kidedea na ushindi wa goli moja kwa sifuri dhidi ya mahasimu wao Timu ya Mpira wa Miguu kutoka Kijiji cha Idodi Kata ya Idodi.
Goli hilo lililowapatia ushindi limefungwa kipindi cha pili cha mchezo huo ikiwa ni dakika ya 70 na Mchezaji anulikanaye kwa jina la huku ubao wa matangazo ukitamatika kusomeka kwa Timu ya Mbugani 1 huku timu ya Idodi 0
Mashindano hayo yalianza kurindima tarehe 30/10/2022 na kutamatishwa terehe12/11/2022 katika Kiwanja cha Michezo Mlowa, huku yakihusisha jumla ya vijiji 28 kutoka Tarafa ya Idodi na Tarafa ya Pawaga, na yakiwa yameandaliwa na Shirika la Uhifadhi Tembo Kusini Mwa Tanzania (Southern Tanzania Elephant - STEP) kwa kushirikiana na Shirika la Uhifadhi Wanyama Walao Nyama (Lion Landscape).
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Mohammed Moyo ameshiriki kama Mgeni Rasmi katika Fainali za Bonanza la Mpira wa miguu kwa Jumuiya za Uhifadhi (Mbomipa) na kushuhudia mtanange huo na kisha kushiriki katika zoezi zima la utoaji wa zawadi kwa washindi.
Mshindi wa kwanza wa Mashindano hayo (Timu ya Mbugani) amezawadiwa kombe la ngao, Mpira wa miguu wenye thamani ya Tsh Elfu Arobaini (40,000/=) pamoja na Kitita cha fedha taslimu Tshs. Laki Tano, Mshindi wa Pili ametoka Tarafa ya Idodi Kata ya Idodi (Timu ya Idodi) na kuzawadiwa mpira wa miguu wenye thamani ya Tshs Elfu Arobaini pamoja na kitita cha fedha taslimu Laki tatu. huku Mshindi wa Tatu akitoka tarafa ya Pawaga Kijiji cha Mbuyuni na kuzawadia Mpira wenye thamani ya Tshs. Elfu Arobaini.
Kauli mbiu ya mashindano haya yalikua ni UHIFADHI WA MBOMIPA KWA MANUFAA YA VIZAZI VYA SASA NA BAADAE.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa