“Tuchague Viongozi Wanaofaa Katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa” – Costantine Kihwele
“Mwaka huu tutakuwa na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa nchi nzima, hivyo tunatakiwa kuchagua viongozi wanaofaa na watakaotuongoza vizuri na kuweza kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi”. Kauli hii imetolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Iringa Komredi Costantine Kihwele, alipokuwa anaongoza kikao cha uwasilishaji wa taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Iringa, ambao ulifanyika Januari 29, 2024 katika Ukumbi wa Siasa ni Kilimo.
Komredi Kihwele ameendelea kusema kuwa, “nitahakikisha kanuni na taratibu zinasimamiwa vizuri na hakuna mjumbe atakayeonewa katika ngazi zote. Hivyo ni jukumu letu kama Chama kuona kila Kata inashinda katika uchaguzi huo”.
Naye Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya Ndugu Rehema Mohamed amesema, “anawashukuru timu ya Wataalam wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Wakili Bashir Muhoja kwa ushirikiano aliotoa katika kufanya ziara Wilaya nzima, tukizunguka Kata kwa Kata. Kwamba kwenye kila mafanikio hapakosi changamoto, hivyo changamoto zote zilizojitokeza tumezichukua na kuziwasilisha ngazi za juu kwa ajili ya utekelezaji zaidi”.
Bi. Rehema pia amewashukuru Taasisi za TARURA, TANESCO, RUWASA NA IRUWASA kwa kushiriki vizuri katika ziara hiyo na kuweza kujibu na changamoto zilizojitokeza na kuzifanyika kazi kwa wakati.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mheshimiwa Veronica Kess, akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani kwa Kipindi cha Miezi sita amesema, “Naishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutulea miradi mingi ambayo ipo hata nje ya Ilani.”
Sasa hivi matokeo ya wanafunzi kwa hatua mbalimbali yametoka na kwamba ufaulu unaridhisha na kwamba wazazi wajitahidi kuhimiza watoto wasome kwa bidii. Matokeo ya wanafunzi imekuwa kama ifuatavyo kwa mwaka 2023 Darasa la Nne Waliondikishwa ni 8,898, Waliofaulu ni 7,149 sawa na 85%, Darasa la Saba waliondikishwa ni 10,471 na waliofaulu ni 9,079 sawa na 88%, Kidato cha Pili waliondikishwa ni 5,413 waliofaulu ni 4,878 sawa na 89% na Kidato cha Nne walioandikishwa ni 4,254 waliofaulu 3,782 sawa na 89% . na Kwamba hadi sasa walioripoti Kidato cha Kwanza ni 5,752. Wanafunzi ziadi ya 3,000 hawajaripoti. Hivyo wazazi wamehimizwa kupeleka watoto shule hata kama na nguo za nyumbani. Watoto walioenda shule binafsi imeagizwa taarifa zao zipelekwe kwake.
Katika Uandikishaji wa Darasa la Awali, waliotegemewa ni 6,643 sawa na 68%, na Waliotegemewa Darasa la Kwanza ni 8,953 na waliondikishwa ni 7,526 sawa na 84%.
Kwa upande wa Watoto wenye mahitaji maalum, Darasa la Awali 29 ambapo Wavulana 16, na Wasichana 13, na Darasa la Kwanza ni 12 ikiwa Wavulana 6 na Wasichana 6. Hivyo kuleta jumla ya watoto wenye mahitaji maalum 41.
Mheshimiwa Kessy ameendelea kusema kuwa, wazazi waendelee kuchangia chakula cha watoto shuleni pia kuchangia ujenzi wa hostel ili kunusuru watoto wanaotoka mbali na shule.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Wakili Bashir Muhoja akijibu hoja zilizoibuliwa na wajumbe katika Mkutano huo amesema, maboma yote yaliyopo ikiwa ni ya zahanati au shule yametengewa bajeti kwa mwaka wa Fedha 2024/2025. Mabomba hayo ni yale ambayo yamefikia hatua tayari yameshapauliwa, Halmashauri kazi yake ni umaliziaji tu.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa