Tanzania Bara inategemea kufanya uchaguzi wa kuchagua viongozi wa Serikali za Mitaa ifikapo Novemba 2024.
Kufuatia tukio hilo muhimu, Tume Huru ya Uchaguzi imekutana na Maafisa Habari wa Mikoa na Halmshauri zote Tanzania Bara Juni 15, katika Ukumbi wa Mlimani City.
Lengo la Mkutano huo ni kukumbushana sheria, kanuni na taratibu zinazopaswa kufuatwa wakati wa kuandika au kusemea masuala yote yanayohusu uchaguzi.
Akiongea katika Mkutano huo Mkurugenzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Ndugi Ramadhan Kailima amesema "Tume inatarajia kupata huduma kwenu za kuchapisha na kujiandikisha na kwamba Tume imeanza mchakato na uzinduzi wake utakuwa Mkoa wa Kigoma Julai 01".
Ndugu Kailima ameendelea kusema, zipo mashine ambazo zimeboreshwa na zinatumia mfumo wa Android na siyo Window tena kama vile vya mwanzo, hivyo uandikishaji utakuwa vizuri bila shida yoyote.
Tume imeomba Maafisa Habari kuepukana na kauli za upotoshaji au kupinga upotoshaji unaotolewa na mtu yeyote kwa nia ya kuiharibia Tume.
Naye Bi. Gladness Aswile Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Elimu kwa Mpiga Kura aliweza kutoa mada inayohusu Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura.
Kadhalika, mada ya pili ambayo ilihusu Mfumo wa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na Vifaa Vinavyotumika ambapo ilitolewa na Mkirugenzi wa TEHAMA wa Tume.
Kauli Mbiu ya mwaka huu inasema, "Kujiandikisha Kuwa Mpiga Kura ni Msingi wa Uchaguzi Bora".
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa