Na Ummi Mohamed(Afisa Habari na Uhusiano Iringa -DC)
Afisa Mwandikishaji wa Uchaguzi Jimbo la Kalenga na Isimani,ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashsuri ya Wilaya ya Iringa Bw Robert Masunya ana wakumbusha Wananchi wote kuwa leo Mei 4 mwaka huu wa 2020 ndio itakuwa mwisho wa zoezi la kuhakiki majina katika Daftari la kudumu la Mpiga kura Awamu ya Pili.
Bw Masunya amewataka wananchi wajitokee kwani kutofanya hivyo watakuwa wamejinyima haki yao ya msingi ya kuchagua Viongozi wao katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
“Nawasihi wananchi waende kuhakiki taarifa zao katika Daftari la Mpiga kura ili kuwawezesha kupiga kura siku ya uchaguzi mkuu mwaka huu”
Rai hiyo aliitoa leo siku ambayo ni ya mwisho katika kuhakiki Daftri la Mpiga kura awamu ya pili zoezi ambalo limedumu kwa siku tatu kuanzia Mei 2 mwaka huu na kufikia tamati leo tarehe 4 ya mwaka 2020.
“Utaratibu huu wa Uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura ni la Nchi nzima sio tu Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Sanjari na zoezi la uboreshaji wa Daftrari ni muhimu wananchi wafikapo katika kituo kufuata maelekezo ya namna ya kujinginga na maambukizi ya CORONA ikiwa ni pamoja na kutokaribiana wawapo vituoni na kuvaa Barakoa kwani Afya ndio msingi wa kwanza na mengine hufuata”Alisisitiza bw Masunya.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa