Maafisa wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi wafika katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Desemba 17, 2024 ili kutoa elimu na kuhamasisha wananchi juu ya zoezi uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura litakalotumika kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 ambapo zoezi la uboreshaji mkoani Iringa linatarajiwa kuanza Desemba 27, 2024 hadi Januari 02, 2025.
Kabla ya zoezi la utoaji elimu na uhamasishaji, maafisa hao wamefanya kikao na Msimamizi wa Uchaguzi wa majimbo ya Kalenga na Isimani Ndg. Robert Masunya, Afisa Uchaguzi wa Halmashauri na viongozi wengine ili kuweka mkakati wa namna ya kufanikisha zoezi hilo.
Kwa upande wake Afisa wa Tume ndugu George Kashura ameeleza juu ya mambo muhimu yanayowekewa msisitizo kwenye utoaji wa elimu hii kuwa walengwa wa uboreshaji huu ambao ni;
Maeneo ambayo yamepitiwa na timu hii ili kupewa elimu na kufanya uhamasishaji ni; Kijiji cha Isakalilo, Kijiji cha Ipamba, Ugwachanya, Wenda, Tanangozi, Ihemi, Ifunda, na Muwimbi katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa