Utekelezaji wa Afua za Lishe Umetumia 68.81% ya Fedha kwa Robo ya Tatu
Kikao cha Tathmini ya Mkataba wa Lishe kimekaa kujadili Taarifa za Robo ya Tatu kwenye utekelezaji wake.
Mratibu wa Lishe Wilaya Bi. Tiliza Mbulla amewasilisha taarifa ya utekelezaji kwa Robo ya Tatu kwenye kikao hicho ambacho kimefanyika Mei 16, 20204 katika Ukumbi wa Halmashauri uliopo Ihemi.
Kamati hiyo inayoongozwa na Mkuu wa Wilaya, imepokea taarifa hiyo na kuwaomba Watendaji wa Kata kuongeza bidii katika ufuatiliaji wa mambo ya lishe kwa wananchi.
Mheshimiwa Kheri amewataka Watendaji wa Kata ambao Kata zao zina alama za hatari katika kutekeleza afua za lishe na kwamba zina alama ya njano na nyekundu, waweze kusisitiza wananchi kufuata kanuni za lishe na sahani ya mfano.
Mheshimiwa Kheri ametumia kikao hicho kuwasisitiza Watendaji kufanya maandalizi mazuri katika mapokezi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru ambao unaratajia kuingia Mkoani Iringa mwezi Juni.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa