“Utoaji Chakula Chenye Virutubisho Shuleni ni la Lazima” – DC Kessy
“Suala la utoaji wa chakula ni lazima na kwamba Watendaji wameomba suala hili liwekwe kwenye Sheria Ndogo za Halmashauri. Wazazi waunde Kamati za ukusanyaji chakula ili kuondoa mkanganyiko wa wazazi/walezi wa kutowaamini Walimu. Chukula kitakachotolewa lazima kiwe na virutubisho ilil kuondoa udumuvu kwa Watoto”. Hii itasaidia watoto kupata muda mzuri kuwa katika masomo yao”.
Kauli hii imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mheshimiwa Veronica Kessy alipokuwa akitoa hotuba fupi kwenye kikao cha Mkataba wa Afua za Lishe kwa Robo ya Tatu kwa mwaka wa Fedha 2022/2023.
Mheshimiwa Kessy amesisitiza kuwa, “nawaomba Waheshimiwa Madiwani tusaidiane kuhimiza wazazi/walezi kuwa ni muhimu chakula kitolewe kwa wingi shuleni. Pia Watendaji wa Kata waangalie usalama na uhifadhi wa chakula kwani ni muhimu sana kwa usalama wa watoto, hivyo wana wajibu wa kusimamia upelekaji wa chakula shuleni.
Aidha Mheshimiwa Kessy ameendelea kusema umuhimu wa lishe na kwamba shule zianzishe bustani za mbogamboga ambazo zitakuwa na tija katika lishe. Pia elimu itolewe juu ya kutunza bustani hizo kwa faida yao wenyewe. Kupanda miti ya matunda kutumia mboga za majani zilizokaushwa katika utaratibu unaotakiwa.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri Mheshimiwa Stephen Mhapa amesema kuwa, “usafi wa mazingira na ujenzi wa vyoo bora ni muhimu sana kwa afya ya jamii yetu, na kwamba utekelezaji wa suala hili utasomwa katika vikao vya kila Robo ili kukumbushana na kuelimishana. Kuna baadhi ya Kata na vijiji bado hazina vyoo bora na kwamba wanajisaidia porini, jambo ambao ni aibu na linatuondolea heshima sana”
Mheshimiwa Mwenyekiti ametoa maaagizo kwa Maafisa Tarafa, Watendaji wa Kata na Vijiji na Maafisa Afya kuwa, katika vikao vyao iwe agenda mojawapo ya kuhamasishana, ili kila nyumba inakuwa na choo bora, na kwamba watakaokuwa wakaidi watatozwa faini.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Ndugu Bashir Muhoja amesema, baada ya shule kufunguliwa atahakikisha chakula kinatolewa kwa wingi na kinakuwa salama. Pia katika ujenzi wa vyoo bora kila Mtendaji asimame kwa nafasi yake ili kuhakikisha kila nyumba ina choo bora.
Naye Mratibu wa Lishe Bi. Avelina Selemani, ameomba kila shule iwe na shamba lake kwani itasaidia kuwa na chakula kingi bila kuwachangisha wazazi, na kuwafundisha watoto elimu ya kujitegemea.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa