Wajumbe wa Kamati ya CAMFED Wilaya ya Iringa (CDC- Iringa DC) wapewa mafunzo yatakayowasaidia kutekeleza majukumu yao kwa weledi na ufanisi. Mafunzo haya yametolewa Agosti 19 hadi 21, 2025 katika ukumbi wa GEF Iringa mjini ambapo wajumbe wapya walioteuliwa watafanya kazi kwa muda wa miaka mitatu.
Akizungumza mara baada ya kuhitimishwa kwa mafunzo hayo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Wilaya Mwl. Alice Nkwera amesema mafunzo haya ya siku tatu yametoa mwongozo kwa wajumbe wapya Kwenda kufanya kazi kwa ufanisi kwani kuna mambo ya msingi yamehimizwa ikiwemo sera ya ulinzi na usalama wa mtoto.
Aidha Mwl. Nkwera amesema Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ni miungoni mwa Halmashauri zinazopokea fedha nyingi za ufadhili wa CAMFED ambapo kwa mwaka 2025/2026 zaidi ya milioni 200 zimetolewa kuhudumia wanafuzi zaidi ya 1,800 kutoka shule 25 kwa mahitaji mbalimbali ya vifaa vya kujifunzia na usafi, sare, huduma ya hosteli nk.
CAMFED ni shirika lisilokuwa la kiserikali linaloshughulika na ustawi wa Watoto na wasichana na kuwa mstari wa mbele katika kuzuia udhalilishaji na ukatili dhidi ya Watoto na na vijana ambao bado ni tegemezi katika familia.
Vile vile inasaidia Watoto hasa wa kike (wasichana) kuweza kumudu masomo na kuboresha mazingira ya kujifunza na kumshika mkono mtoto wa kike kwenye hatua mbalimbali kupitia progaramu zake za elimu ya wasichana, mpango wa learner guide, CAMFED Association (CAMA), na msaada wa baada ya shule.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa