Wanakwaya Kutoka Tabora Wafurahia Vivuti Iringa DC
Afisa utalii wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Bwana Abinery Msovela amewaongoza Watalii 48 kutoka Tabora Evangelist Chor (TEC) kufanya Utalii wa Ndani kwenye vivuti vilivyopo Iringa, kama Kikongoma na Makumbusho ya Mkwawa Kalenga.
Afisa Utalii huyo amewapongeza na kuwashukuru kwa kuchagua Iringa kufanya utalii wa ndani maana ni historia inajengwa kwa vizazi na vizazi na akiwaomba kuwa Mabalozi wazuri wa kuhamasisha utalii wa ndani.
Erick Jordan Muhifadhi Mali Kale Mkuu wa Kituo cha Makukumbusho ya Mtwa Mkwawa Kalenga, amewashukuru kwa kuchagua kituo cha Kaqlenga na kuwaeleza historia ya chimbuko la Wahehe.
Vilevile Mchungaji wa Kanisa hilo Emanuel Mabula amdesema wamekuja huku kujifunza asili ya Wahehe na kujua taratibu za kabila hilo kwa ajili ya kumbukumbu pia kama walifika Iringa.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa