“Wananchi ni Wajibu Wetu Kumunga Mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania” – Daud Yassin
Kauli hii imetolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Iringa Komredi Daud Yassin Mlowe alipokuwa katika ziara ya Kamati ya Siasa Mkoa Januari 27, 2024.
“kutokana na Rais wetu kujali wananchi wake kwa kuleta miradi mbalimbali kama shule barabara, zahanati na hospitali, sisi wananchi kazi yetu ni kumuunga mkono Mheshimiwa Rais katika kila jambo analofanya”
Kamati hiyo imeweza kutembelea miradi mbalimbali katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa na kujionea shughuli za miradi inayotekelezwa katika Halmashauri hiyo.
Shule mpya ya Sekondari ya Mbaliboli iliyopo katika Kata ya Mboliboli, Shule mpya ya Sekondari ya Weru iliyopo katika Kata ya Ulanda na Hospitali Teule ya Tosamaganga iliyopo Kata ya Kalenga.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mheshimiwa Halima Omary Dendego amesema, “namshukuru mwananchi aliyetoa eneo lake kwa ajili ya kujenga shule ya Weru. Huu ni uzalendo kwa nchi yake na kupenda maendeleo. Hivyo kwa ajili ya kumuenzi mwananchi huyu naomba jina la shule libadilike badala yakuitwa Weru shule iitwe Sambala, ambapo ndiyo jina la mwananchi aliyejitolea eneo hili”.
Kamati imeridhia kwa kutoa jina hilo na kuahidi matatizo mengine ya shule hiyo ambayo bado yapo, kama bweni hasa kwa watoto wa kike ambao bado wanatoka mbali na eneo hilo.
katika taarifa ya hospitali ya Tosamaganga Mkurugenzi wa Hospitali hiyo Ndugu Benjamin Mfaume pia amewasilisha ombi la kutokatiwa umeme kwani mashine iliyonunuliwa ya mionzi (CT Scan) inatumia umeme mwingi sana. Pia ombi la kujengewa Kituo cha Polisi kwani usalama wa eneo hilo ni mdogo kwa wagonjwa na wauguzaji.
Aidha, Mtaalamu wa mionzi Sr. Aristridia Muhafi aliweza kutoa maelezo jinsi mashine hiyo inavyofanya kazi.
Pia kamati imefurahishwa sana na huduma zitolewazo katika Hospitali ya Tosamaganga, kwani imekuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa Iringa na wananchi wanaotoka nje ya Mkoa.
Kwa kuwa ilikuwa ni siku ya upandaji miti Duniani, Viongozi hao walipata nafasi ya kupanda miti katika Shule Sekondari Weru kwa ukumbusho zaidi.
Mwenyekiti aliweza kuwashukuru wananchi, Madiwani na Uongozi wa Halmashari kwa kuweza kushirikiana katika kutekeleza miradi hiyo.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa