Wananchi wa Mgega Wafunguliwa Njia na ASF
Assist Small Farmers (ASF) ni Shirika lisilo la Kiserikali linaloshughulika na kuwasaidia wakulima wadogo kukuza kilimo chao.
Katika kuhakikisha mwananchi na mkulima mdogo ananufaika Shirika la ASF limedhamira kutambulisha mradi ambao utarahisha maisha kwa wananchi, wakinza kwa kujenga madarasa mawili katika Kitongoji cha Mgega Kijiji cha Mfyome Kata ya Kiwele ambako kuna Shule Shikizi.
Akitambulusha mradi huo Ndugu Datan Ndunguru Meneja wa Shirika amesema, wanahakikisha wakulima wanapata maendeleo, mkulima afanye kilimo chenye tija kwa kuwawekea huduma za kijamii kama maji, kujenga vyoo na kulima mbogamboga ambazo zitasaidia katika lishe.
Kijiji cha Mfyome kuna wananchi jamii ya Kimasai ambao wameanzisha makazi eneo hilo na hakuna huduma za kijamii. Hovyo basi kama shirikia wameona watoe huduma hizo na hasa kilimo ili kujiongezea kipato na kukuza uchumi.
Pia kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maji Vijijini (RUWASA) watachimba visima ili kukidhi mahitaji ya maji safi na salama. Kwa kuweka bustani ya mbogamboga (Gren House) watawauzia wananchi pia waige mfano huo wakalime katika jamii zao.
Mradi huo utagharimu kiasi cha Milioni 114 za Kitanzania.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa