Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi wa ngazi ya kata katika Jimbo la Kalenga na Ismani wapatiwa mafunzo kutoka kwa wataalamu wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi mapema Agosti 04, 2025 katika Ukumbi wa Shule ya Wasichana Ifunda.
Akifungua Mafunzo hayo Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Kalenga na Ismani Bi. Caroline Ang’wen Otieno amesisitiza washiriki wa mafunzo kusoma Katiba, shria, kanuni, taratibu na miongozo mbalimbali inayotolewa ili kuwarahisishia katika utekelezaji wa majukumu yao.
“Someni kwa umakini Katiba, sheria, kanuni, miongozo na maelekezo mbalimbali yaliyotolewa na yatakayotolewa na Tume na ulizeni ili kupata ufafanuzi wa maeneo ambayo kwa namna moja au nyingine pengine yatakuwa na changamoto ili kuwarahisishia katika utekelezaji wa kazi wakati wa uchaguzi” Amesema Bi. Otieno.
Sanjari na mafunzo hayo, vilevile washiriki wa mafunzo wapatao, 56 kutoka kata 28 za majimbo yote mawili ya Halmashauri ya Wilaya ya Iringa wamekula viapo vya kutunza siri na kujitoa uanachama wa vyama vya siasa ili kukidhi matakwa ya kisheria.
Mafunzo haya yana lengo la kujenga uwezo kwa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya Kata (ARO KATA) ili kuwa na uwezo wa kufanya kazi kwa uadilifu, weledi na kwa kuzingatia sheria na kanuni zilizowekwa.
Kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025, tunasimamia kauli mbiu isemayo, “Kura ni Haki yako, Jitokeze Kupiga kura”
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa