OFISI YA RAIS
|
|
|
|
TAARIFA KWA UMMA
WANAFUNZI 4,374 KUFANYA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2023
Jumla ya Watahiniwa 4,374 wa Kidato cha Nne katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, wameungana na wenzao nchini kote kufanya mtihani wa kuhitimu Kidato cha Nne mwaka 2023 ambao unafanyika kuanzia Jumatatu Novemba 13, 2023.
Kati ya Watahiniwa hao 4,374, Wavulana ni 1,884 na Wasichana 2,500, ambapo Watahiniwa wa Shule ni 4,355 (Wavulana 1,874 na Wasichana ni 2,481) , Watahiniwa wa Kujitegemea ni 19 (Wavulana 10 na Wasichana 19). Watahiniwa wa mtihani wa Maarifa (QT) ni 2 (Mvulana ni 1 na Msichana 1), na jumla ya vituo vya kufanyia mitihani ni 42.
Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa unawatakia kila la kheri watahiniwa wote wa Kidato cha Nne 2023 katika mitihani yao ya kuhitimu elimu ya Sekondari na kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu wafanye vyema na huku wakizingatia taratibu zote za mitihani.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Halmashauri ya Wilaya ya Iringa,
Novemba 13, 2023.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa