Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Wakili Bashir Muhoja wamfanya kikao kazi na Watendaji wa kata na vijiji katika Halmashauri mapema tarehe 17.11.2023 ili kuangalia hali ya utendaji, usimamizi wa miradi na ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri.
Akizungumza wakati wa kikao Wakili Bashir Muhoja amesema, Halmashauri inatarajia kupokea fedha za miradi na zingine tayari zimeshaingia hivyo tunatakiwa tukimbizane nazo ili kufikia mwezi Machi tuwe tumemaliza miradi yote ambayo tumeletewa. Na kwamba fedha za miradi zinapoingia watendaji wanapaswa kishirikiana na wataalamu wengine ili utekelezaji wa miradi uwe wa haraka badala ya kuwaachia wataalamu wengine kama walimu.
Kwa upande wa ukusanyaji wa mapato, Wakili Muhoja amesema lazima kila mmoja awajibike kubaini maeneo yenye uwezekano wa ukusanyaji mapato kwa kutoa taarifa kimaandishi kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ili yaweze kufanyiwa kazi kwani ukusanyaji wa mapato unapaswa kufanywa kwa umoja kama timu.
Pia ameongeza kuwa Halmashauri ipo kwenye hatua ya mwisho kununua POS ili zisambazwe kwenye kila kijiji ili kusiwe na kisingizio chochote cha kutokuwa na POS.
Naye Naye Kny. Mkuu wa Kitengo cha Viwanda, Biashara na Uwekezaji ndg. Riziki Mhagila ametoa ufafanuzi wa namna ya kutuma maombi ya leseni hatua kwa hatua hadi kupata hati ya leseni na kuongeza kuwa Watendaji lazima watoe ushirikiano wa kuhakikisha kuwa watu wasio na leseni wala vitambulisho vya mjasiriamali walipe ushuru hasa kwenye maeneo ya minada. Pia wafanyabiashara wa bajaji na bodaboda wanapaswa kupata leseni ya usafirishaji ambayo inatolewa Halmashauri kwa niaba ya LATRA.
Kwa upande wake Mhandisi wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Eng. Kasiririka ametoa vigezo vya utoaji wa vibali vyote ya ujenzi na hatua za upatikanaji wake na kuhimiza kuwa kila anayetaka kujenga lazima awe na kibali cha ujenzi na kwamba watendaji wanapaswa kuhafanya uchunguzi wa majengo yanayojengwa ili kubaini kama wanaojenga wana vibali.
Vilevile Mkuu wa Idara ya Utawala na Rasilimali watu wa Halmashauri Bi. Beatrice Augustino amesisitiza juu ya suala zima la utawala bora na kuhimiza kuwa watendaji lazima wahakikishe kuwa vikao na mikutano ya kisheria inafanyika kwa wakati na mihutasari yote imfikie Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri. Sanjari na hayo pia ameweza kupokea changamoto za kiutumishi zinazowakuta watendaji na kuzitolea ufafanuzi wake ikiwemo maslahi na stahiki za watumishi hasa watendaji wa kata na vijiji.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa