Waliojengewa uwezo kuhusu mfumo wa Nest ni watendaji wa vijiji, watendaji wa kata, walimu wakuu, wakuu wa shule, waganga wafawidhi wa zahanati zote na vituo vya afya na maafisa ununuzi wa ngazi mbalimbali
Watumishi zaidi ya 868 kutoka ngazi za kutolea huduma (Lower-level Government Procuring Entities) katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa wapewa mafunzo ya kuwajengea uwezo kwenye mfumo wa ununuzi wa Umma (Nest), mafunzo ambayo yametolewa na Ofisi ya Mamlaka ya Uthibiti wa Ununuzi wa Umma yaliyofanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo na shule ya sekondari Lugalo Februari 26 na 27, 2025.
Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Ndugu Robert Masunya amesema, “Serikali imewekeza kiasi kikubwa sana ambacho kinakuja kwenye maeneo tunayoyasimamia sisi, kwa hiyo Serikali ikaamua kuwa na mfumo sahihi wa kuwapata watoa huduma na kutoa mwelekeo wa usimamizi wa shughuli za miradi niwaombe kuwa makini sana kwenye mafunzo haya”.
Aidha Ndugu Masunya amewatahadharisha washiriki wa mafunzo juu ya umuhimu wa kutumia mfumo katika manunuzi ya umma na kwamba kuna adhabu kwa watakaofanya manunuzi bila kutumia mfumo.
Kwa upande wao wakufunzi wa mfumo wa Nest wakati wa mafunzo wameeleza umuhimu wa kutumia mfumo wa Nest katika manunuzi ya Umma na namna ya kuutumia mfumo hatua kwa hatua sanjari na kutoa usaidizi juu ya changamoto mbalimbali kuhusu matumizi ya mfumo.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa