“Viongozi wa Iringa Mtabarikiwa kwa Kuwajali Wazee”, Dkt Biteko
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mheshimiwa Dkt. Doto Mashaka Biteko, amewapongeza Viongozi Mkoani Iringa kwa kuwajali na kuwenze Wazee na kuthamini mchango wao katika maendeleo ya jamii.
Dkt. Biteko ameyasema hayo Oktoba 03, 2023 mara baada ya kupokelewa na viongozi hao katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Aidha Dkt. Biteko amesema kuwa katika jamii yoyote ile wazee ni wa muhimu katika mambo mbalimbali.
“Naongea kama mtu niliyefundishwa dini na siyo kama kiongozi wa dini, hivyo niwaambie tu viongozi wa Mkoa wa Iringa mtabarikiwa”, amesema Dkt Biteko.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa