Azitaja hudumazinazotolewa hapo na kuzipongeza taasisi za dini kwa kuunga mkono jitihada za serikali kutoa katika jamii ikiwemo huduma ya afya.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amefanya uzinduzi wa Hospitali ya Teule ya Tosamaganga kuwa Hospitali ya Rufaa ngazi ya Mkoa (Tosamaganga Regional Referral Hospital) Julai 06, 2024.
Akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi, Mhe. Majaliwa amelipongeza kanisa kwa jitihada za kupandisha hadhi Hospitali teule ya Tosamaganga kuwa Hospitali ya Rufaa ngazi ya Mkoa ambapo katika Mkoa wa Iringa tayari kumeshakuwa na Hospitali mbili za rufaa zenye uwezo wa kutoa huduma za kibingwa, hivyo kupunguza adha ya wananchi kusafiri hadi Dodoma au Dar es salaam kufuata huduma hizo.
Aidha Mhe. Majaliwa amezitaja huduma zinazotolwa katika Hospitali ya Rufaa ya Tosamaganga kuwa ni; Huduma ya Uzazi na magonjwa ya mfumo wa uzazi wa akinamama, Upasuaji wa mifupa, huduma ya upasuaji wa jumla (general surgery), Huduma ya wagonjwa wa nje (OPD), huduma ya wagonjwa wa magonjwa yasiyoambukiza, huduma ya wagonjwa wa dharura (Emergrnce department), idara ya mionzi, huduma ya wagonjwa wa mfumo wa ubongo na mishipa ya fahamu, huduma ya kinywa na meno, huduma ya idara ya watoto, huduma ya utenganifu wa matibabu ya figo, na huduma ya wagojwa wa magonjwa ya ngozi,
“Dhamira ya Rais Dkt. Samia ni kuwatumikia wananchi kwa kuhakikisha sekta ya afya inafika kila mahali ikiwemo kujenga Hospitali kwenye kila halmashauri. Watanzania endeleeni kuwa na Imani na serikali yenu, nasi tutaendelea kuwahudumia ipasavyo” amesema Mhe. Majaliwa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Tosamaganga amesema, hospitali inatoa huduma za kibingwa na bobezi hivyo kkuweza kuchangia kwa kiasi kikubwa kuboresha afya za watanzania. Pia ametoa shukrani kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa msaada wa hali na mali unaotolewa kwenye hospitali.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa