Waziri Kairuki agiza wawekezeji Halmashauri ya Wilaya ya Iringa wapelekewe Huduma ya Umeme.
Na Ummi Mohamed (Afisa Habari na Uhusiano,Iringa –DC)
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu;Uwekezaji Mh. Angellah Kairuki ameiagiza Tanesco kupeleka huduma ya Umeme kwa wawekezaji waliopo ili kuwapunguzia gharama za uzalishaji na uendeshaji wa Kampuni zao.
Kauli hiyo aliitoa alipofanya majumuisho ya ziara yake ya kikazi katika Halmashauri ya Wiliya ya Iringa ambapo aliokea Changamoto hiyo kutoka kwa wawekezaji wa Shamba la mifugo la Kampuni ya Asas lililopo Kijiji cha Nyang’oro na Kamupuni ya Masifio iliyopo Kijiji cha Bandabichi.
Aidha changamoto hiyo iliwasilishwa na Wakurugenzi wa Makampuni hayo wakati wakisoma taarifa fupi ya uwekezaji wao kwa Mh Waziri , na kuelezaji jinsi gani wanashindwa kusonga mbele kutokana na changamoto hiyo.
Baada ya kuona Changamoto kubwa inayowakabili wawekezaji hao inafanana ndipo alipoiagiza Tanesco mkoa wa Iringa kuhakikisha huduma hiyo inawafikia kwa haraka kama ambavyo Serikali imekuwa ikiwaahidi wananchi wake.
“Nagiza Shirika la Umeme Mkoani Iringa kufikisha umeme kwa Wawekezaji wa Kampuni ya Masifio iliyopo Kijiji cha Bandabichi na Shamba la ASAS lililopo katika Kijiji cha Nyang’oro ili kuwawezesha wawekezaji hawa kuongeza ufanisi katika uzalishaji ili kuongeza ajira kwa vijana wetu wa Kitanzania” aliongeza kuwa;
“Nimesikia tena na hapa katika taarifa fupi muwekezaji anatumia zaidi ya milioni moja kwa wiki kununua mafuta ya jenereta ili aweze kuendeleza shughuli zake za uzalishaji lakini Juni 22 pia nilipokea changamoto hii kutoka Kampuni ya Asas, kwa kuwa Tanesco mpo katika ziara hii naomba mlifanyie kazi kwa haraka na nitarudi ili kuona limefikia wapi suala hili”alisema Waziri Kairuki.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Bw.Quentin Robb ameishukuru sana Serikali ya awamu ya tano kwa kada zote kwa jinsi inavyowatendea vyema wawekezaji wa ndani na nje kwa usawa.
Naye Mkurugenzi wa kiwanda cha maziwa cha ASAS Fuad Abri aliipongeza Serikali kwa kufanya ziara zake mara kwa mara na kupita katika kiwanda chake hali inayopelekea kuona jinsi gani Serikali inawajali na kuwathamini wawekezaji wote.
.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa