Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Bw Robert Masunya ameteua baadhi ya Majengo ya Zahanati ya Kising'a kuwa kituo maalum kwa ajili ya Wagonjwa wa Corona iwapo watatokea katika Halmashauri yake.
Bw Masunya amesema mpaka sasa hakuna mgonjwa aliyethibitika katika halmashauri yake.
Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii jinsia Wazee na Watoto imetoa Gari ya kubebea Wagonjwa yenye thamani ya Milioni 120 kwa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.
Akipokea gari hiyo Bw Robert Masunya ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauriya Wilaya ya Iringa amesema gari hiyo itasaidia kuokoa misha ya watu wengi hasa kwa wakina mama na watoto.
Mwnyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Mh Stephan Mhapa ametoa rai kwa wajumbe wa Baraza la Madiwani kushiriki katika kutoa elimu dhidi ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa homa ya Mapafu (COVID19) kwa wananchi ili waendelee kutokuwa na maambukizi ya ugonjwa huo.
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa